Jumatano , 9th Feb , 2022

Video ya mchungaji mmoja kutoka nchini Ghana imesambaa mitandaoni ikimuonesha akiwalambisha vidole vyake waumini mara baada ya yeye kula chakula kwa madai ya kwamba anawapatia komunio.

Mchungaji akiwalambisha vidole waumini wake

Mchungaji huyo pia haishiwi vioja baada ya siku ya mwaka mpya wa 2022 video yake ilisambaa mitandaoni ikimuonesha akiwavua nguo, kuwaogesha na kuwapaka mafuta wanawake kwa kudai kwamba hayo yalikuwa ni maelekezo aliyopewa na roho mtakatifu.