Alhamisi , 11th Sep , 2025

Hii ni baadhi ya miji nchini Marekani ambayo ina idadi kubwa zaidi ya watu wenye asili ya Afrika wengi tumezoea kuwatambua kama (Afro-America)

1. Mound Bayou, Mississippi - Taarifa inaonyesha wakazi wengi ni wenye asili ya ‘’Afro-America’’

- Idadi ya watu wote kwenye mji huu ni 1,394 mpaka kufikia mwaka (2024)

- Ulianzishwa July 12, mwaka 1887

- Watu weusi ni 96.8% ya wakazi wote

2. Grenada, Mississippi

- Watu weusi ni wengi kuliko makundi mengine, mfano mwaka 2020 waliongezeka hadi kufikia 12,700

- Mji huu ulianzishwa mwaka 1836

- Takriban 70% ya watu ndani ya mji huu ni weusi, hasa katika maeneo ya miji kama Grenada

3. East St. Louis, Illinois

- Watu weusi ni 95.35% ya jumla ya mji (takriban watu 17,428)

- Ni moja ya miji yenye idadi kubwa ya watu weusi Marekani

- Wachache sana ni makundi mengine kama Weupe (1.63%) na Wahispania (1.40%)

Kwa ufupi: Miji hii mitatu ina idadi kubwa sana ya watu weusi, kuanzia 95% hadi 97% ya jumla ya watu.