Jumatatu , 22nd Jan , 2024

Shania Muhammad, mwenye umri wa miaka 16 kutoka Oklahoma City ameweka rekodi ya kuwa mwalimu mwenye umri mdogo zaidi kwa nchini Marekani, akifundisha wanafunzi wa darasa la tatu kwenye mji wa Oklahoma.

Shania Muhammad alihitimu chuo akiwa na miaka 15 (huyu ndiye mwenye digrii 3) na kwa sasa akiwa bado ni mwalimu anaendeleza safari yake ya maajabu kitaalamu kwa kusoma shahada ya uzamili katika maswala ya biashara.