Mwanamke amshambulia Polisi kwa kumng'oa sikio

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Afisa mmoja wa Polisi huko nchini Kenya ameshambuliwa na mwanamke kutoka eneo la  Lang'ata Jijini Nariobi, kwa kung'atwa hadi kutolewa sikio lake wakati wa purukushani kati yake na mwanamke huyo.

Gari la Polisi nchini Kenya

Taarifa zinadai kuwa Mwanamke huyo alimshambulia Polisi baada ya kuulizwa kwanini amekaa nje baada ya saa mbili usiku ndipo wakaanza kurushiana maneno kisha akamrukia Polisi na kumshika kichwa chake kwa nguvu na kumng'ata sikio hadi kuling'oa.

Ripoti ya Polisi inaeleza kuwa "Baada ya kugundua amemjeruhi afisa huyo, alikimbilia katika mto unaopakana na Lang’ata na Kibera, Sajini huyo aliokota sikio lake ambalo lilikuwa limeanguka na kuelekea hadi Hospitali ya Nairobi West”.

Aidha ripoti hiyo imeendelea kwa kusema uchunguzi kuhusiana na kisa hicho unaendelea huku Afisa huyo wa Polisi akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza sikio lake.

Chanzo : Citizen Tv