Mzazi atupa mtoto mchanga kwenye daraja

Alhamisi , 20th Jun , 2019

Wasamalia wema wamemuokoa mtoto mchanga, ambaye alitupwa na mzazi wake muda mfupi baada ya kuwa amezaliwa katika daraja lililopo kijiji cha Mtisi kata ya Sitalike wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi.

Mtoto Neema

Baada ya kumuokoa, raia hao wema walimpeleka katika hospitali ya mkoa wa Katavi ambako hali yake ya afya kwa sasa inaendelea vyema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa hospitali  teule ya Mkoa, muuguzi  James Kasabanga, amesema kuwa mtoto huyo wamempokea akiwa katika hali mbaya, ila kwa sasa anaendelea vizuri na amewaomba wasamalia wema kujitokeza kumsaidia mtoto huyo kwani ana uhitaji wa mahitaji muhimu.

Kutokana na jinsi walivyoweza kuokoa uhai wake ,Suzan Tarimo ambaye ni muuguzi katika hospitali hiyo, amesema mtoto huyo wamempa jina la Neema kwa sababu ameokolewa kwa Neema ya Mungu.
 

Zaidi tazama Video hapo chini