Ndani ya ubongo wa Bill Gates

Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Kupitia akaunti yake ya 'Twitter',  Bill Gates ametanabaisha juu ya ujio wa dokumentari ambayo itakuwa na sehemu mbili iliyopewa jina la Inside Bill’s Brain: Decoding Bill Gates.

Bill Gates

Dokumentari hiyo itaangazia maisha yake ya nyuma, sasa na mipango ya baadaye pamoja na kuangazia changamoto mbalimbali alizokumbana nazo.

"Nimetumia miaka ya hivi karibuni kufanikisha ujio wa dokumentari hii ambayo inatarajiwa kuachiwa rasmi Septemba 20 ikiangazia maisha yangu pamoja na kazi, nina imani mtafurahia kile kilichofanyika," ameandika Bill Gates.

Kwa mujibu wa Forbes, Bill Gates kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa watu matajiri zaidi duniani akitajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya pesa za kitanzania Trilioni 222. (FB & WEB).