"Pasaka sio kula pilau" - Askofu Wiliam Mwamalanga

Ijumaa , 2nd Apr , 2021

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binaadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu Wiliam Mwamalanga amesema kusheherkea siku ya Pasaka sio kula pilau na ulevi bali ni siku ya kutulia na kujifunza kutoka kwa Mungu.

Askofu Wiliam Mwamalanga

Askofu William Mwamalanga amesema siku ya Pasaka Mungu amedhibitisha kuwa binaadam si lolote wala chochote kwenye dunia hii.

"Pasaka ya mwaka huu itakuwa na maana kubwa sana kwa watanzania, Pasaka sio kula pilau, kutafuta bia na ulevi vitu hivyo ni kinyume, maana ya Pasaka ni kutulia na kujifunza maana Mungu anadhibitisha kwamba binaadam si lolote na si chochote na unaishi kwa maisha ambayo umeyaazima, tofauti na Yesu alivyosema nitakufa na siku ya tatu nitafufuka"  ameeleza Askofu William Mwamalanga