Programu ya kubadili sura 'FaceApp' kuchunguzwa

Ijumaa , 19th Jul , 2019

Kufuatia programu inayobadilisha muonekano wa mtu na kuonesha namna atakavyokuwa mzee, maarufu 'FaceApp' kupendwa na kutumiwa na watu wengi duniani, nchi ya Marekani imetaka uchunguzi zaidi wa programu hiyo.

Programu ya FaceApp

Agizo la kuchunguzwa kwa programu hiyo limetolewa na Seneta mwandamizi katika Jiji la New York nchini humo, Chuck Schumer, ambapo amekiagiza kitengo cha uchunguzi wa ndani na ulinzi (FBI) kuichunguza programu hiyo kufuatia kile alichokidai ni tishio la kiusalama.

Seneta huyo amedai kwamba programu hiyo inamilikiwa na kampuni ya nchini Urusi, ambako ndiko yaliko makao yake makuu na kudai kuwa kuna uwezekano wa kutokea hatari kwa watumiaji wake, ikiwemo kudukuliwa taarifa zao.