Ripoti mpya ya taarifa kuhusu kifo cha George

Jumanne , 2nd Jun , 2020

Taarifa mpya kuhusu kifo cha raia George Floyd ambaye ameuliwa na polisi Derek Chauvin wiki iliyopita inaeleza kuwa, marehemu alipatwa na mshtuko wa moyo na kufeli kwa mishipa ya damu wakati alivyokamatwa na polisi huyo.

Baadhi ya waandamanaji wakishika mabango yanayoeleza kutaka haki kuhusu kifo cha George Flyod dhidi ya polisi

Ripoti hiyo imetolewa na kituo cha matibabu cha  "The Hennepin County Medical Examine" kimeongeza kusema wamegundua marehemu George Floyd siku za karibuni kabla ya kifo chake alikuwa anatumia madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine.

Pia ripoti imeendelea kueleza kuwa aina ya sababu ya kifo chake ni mauaji, ambapo polisi alimkandamiza kwa kutumia goti lake  shingoni mwa George Floyd hadi kufariki.

Kwa upande wa mwanamichezo tajiri duniani Floyd Mayweather amejitolea kulipa huduma na gharama zote za mazishi ya George Floyd siku ya Juni 9, 2020 yenye ya thamani ya Tsh Milioni 204, kwenda kwenye miji mitatu tofauti ambayo ni Houston, Minnesota, na Charlotte nchini Marekani.

Kwa sasa polisi ambaye amefanya tukio hilo  Derek Chauvin na wenzake wanne wamefukuzwa kazi huko Minneapolis, Marekani kisha  kukabiliwa na kesi ya mauaji ya juu "First degree murder"