Jumatano , 26th Oct , 2022

Oktoba 17 mwaka huu kampeni ya Namthamini ilifika katika mkoa wa Njombe kwa ajili ya kugawa taulo za kike kwa wanafunzi mashuleni sambamba na kutoa elimu ya hedhi salama pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiamini wakiwa katika kipindi cha hedhi.

Mtangazaji wa East Africa TV na Balozi wa Kampeni ya Namthamini, Najma Paul akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari Uwemba.

Shule 6 kutoka wilaya tatu za Njombe Mji, Makete na Ludewa zilifikiwa na kampeni ya Namthamini ambazo ni shule za Sekondari Iwawa, Kitulo, Mabatini, Uwemba, Mavala na Mchuchuma.

Shule ya Sekondari Iwawa na Kitulo katika wilaya ya Makete zilipatiwa taulo za kike jumla ya pakiti 1512.

Wilaya ya Njombe Mji kampeni ya Namthamini ilifika katika shule ya Sekondari Mabatini pamoja na shule ya Sekondari Uwemba.

ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 2040 zilitolewa kwa shule zote mbili.

Wilaya ya Ludewa kampeni ya Namthamini ilifika katika shule ya Sekondari Mavala na Mchuchuma ambapo wilaya hii ilipatiwa taulo za kike pakiti 1658.