Jumanne , 31st Oct , 2023

Wasanii wa Afrobeat kutokea nchini Nigeria mwaka huu 2023 wameshiriki kutoa burudani kwenye matukio mengi makubwa.

Wasanii wa Nigeria

Burna Boy alifanya show kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) kati ya Manchester City na Inter Milan iliyofanyika nchini Uturuki June 10, 2023

Tiwa Savage alitumbuiza kwenye sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza, Mei 8 mwaka huu.

Davido alipiga show kwenye utolewaji wa tuzo za BET zilizofanyika nchini Marekani mwaka huu.

Na usiku wa kuamkia leo Heis Rema alitumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za Ballon d’Or zilizofanyika nchini Ufaransa.