Wavamia eneo la Makaburi na kufanya makazi

Ijumaa , 25th Jan , 2019

Wakazi wa mtaa wa Pakacha, Tandale jijini Dar es salaam wamelalamikia eneo la Itongo  katika mtaa huo lilitengwa maalum kwa ajili ya maziko ya watu kuvamiwa na watu na kuanza ujenzi wa makazi.

Pichani wakazi wa eneo hilo.

Wakiongea na KURASA, wananchi hao wameeleza hofu waliyonayo ya ujenzi huo kama utakuwa endelevu kuwa miili ya marehemu hao inaweza ikafukuliwa na kukosa mahala pa kuhifadhiwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Pakacha, Bw. Kasim Omari amesema ameshatoa maelekezo juu ya ujenzi unaoendelea katika eneo hilo la makaburi na kwamba hakuna mwili wa marehemu, uliohifadhiwa katika makaburi hayo utakaofukuliwa kutokana na ujenzi.

"Eneo lile lilikuwa ni la familia na wanaojenga ni wanafamilia, hivyo hakuna uvamizi wowote lakini, nimeshatoa maelekezo wasiendelee kujenga katika eneo hilo", amesema Mwenyekiti huo.

Akiwa mkoani Kilimanjaro mwaka jana Waziri wa Ardhi, William Lukuvi alipiga marufuku, watu kufanya maziko majumbani badala yake watumie maeneo yaliyotengwa na serikali.

Bofya link hapo chini kutazama eneo hilo.