Yule wa 900 itapendeza bado anangoja mabilioni

Ijumaa , 18th Oct , 2019

Tajiri matata aliyewahi kuvuma na msemo wa 900 itapendeza, Dkt Louis Shika, amesema kuwa hadi sasa bado anaendelea kungoja pesa zake, ambazo anazisafirisha kwa njia ya posta.

Tajiri mtata Dkt Louis Shika

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Oktoba 18, 2019, Dkt Shika, amekitaja kiasi anachokitarajia kukipata kwamba ni kiasi cha dola za Marekani bilioni 11.

''Ninashauri kwamba tufanye siku nyingine kwasababu sasa hivi ninapoongea hapa nipo Posta nashughulikia masuala hayo hayo na kiasi cha pesa ninachokitegemea  ni Dolla za Kimarekani bilioni 11 na niko ofisi husika za malipo, nipo namsubiri mwenzangu afike'' amesema Dkt Shika.

Dkt Shika alijizolea umaarufu huo mwaka 2017, wakati wa zoezi la upigaji mnada wa nyumba za Lugumi, baada ya yeye kupanda dau hadi kufikia kiasi cha Shilingi milioni 900 na baadaye alipohojiwa yeye alidai kuwa hakusema milioni 900 bali alitamka 900 itapendeza zaidi.