Jumamosi , 7th Sep , 2019

Baada ya kuachia ngoma ya Bugana, wasanii Billnas na Nandy, wamekuwa wakitrend sana mitandaoni wakitajwa kurudiana, japo wao wamekuwa wakikanusha hilo.

Nandy na Maua Sama

Baada ya kuingia kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, wawili hao wameweka wazi kuwa wamefanya kazi tu huku Billnas akisema Nandy ni mdogo wake kama Maua Sama, lakini Maua akagoma kuwa yeye hahusiki kwenye huo mchongo.

Mbali na hilo Maua Sama ameweka wazi kuwa kuna ngoma nyingi sana, alikuwa anafikiria kuzitoa lakini anaogopa kutokana na ngoma zilizopita kufanya vizuri hivyo alikuwa anatafuta 'Come Back' na mwisho ameipata kwenye 'Niteke'.

Zaidi tazama Video hapa chini