Jumatano , 2nd Mar , 2022

Mmiliki wa klabu ya chelsea Roman Abramovich ameiweka rasmi sokoni timu hiyo na ameiagiza benki ya Marekani ya Raine Group kushughulikia na kusimamia mauzo ya Chelsea.

(Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovic)

Inafahamika kuwa Mrusi huyo amewalenga wanunuzi wa Marekani kwani uwekezaji kutoka China, Mashariki ya Mbali na Ulaya Mashariki umekua mgumu kwa sababu za kisiasa, ingawa kuna shaka kubwa kwamba mnunuzi yeyote atalazimika kufikia thamani ya paund billioni 3.

(Bilionea wa Uswissi Hansjorg Wyss akiwa na mkewe)

Roman Abramovich anaogopa kuwekewa vikwazo zaidi na kuuza mali zake alizowekeza Uingereza, mmoja kati ya watu wanaopigiwa chapuo kuinunua klabu hiyo ni billionea wa Uswissi Hansjorg Wyss, ambaye alisema yeye na watu wengine watatu wamepokea ofa ya kupewa kipaumbele cha kuinunua Chelsea kutoka kwa Abramovich.

Bilionea hiyo wa Uswizi Hansjorg Wyss anadai kuwa amepewa nafasi ya kuinunua Chelsea, tangu bunge la uingereza lilipohoji kwamba Roman Abramovich atalazimika kuuza mali zake alizowekeza Uingereza kwa haraka iwezekananvyo.

Mwekezaji huyo mwenye umri wa miaka 86 amekiri kutaka kuinunua klabu hiyo ya Stamford Bridge kutoka kwa Abramovich, kama sehemu ya muungano wao kibiashara.