Jumanne , 19th Jan , 2021

Inaripotiwa kuwa beki wa Bayern Munich David Alaba amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania mwishoni mwa msimu huu pindi atakapomaliza mkataba na miamba hiyo ya Ujerumani na atasaini mkataba wa miaka 4 na Los Blancos.

David Alaba ameshinda jumla ya mataji 23 na kikosi cha the Bavarians tangu alipojiunga na kikosi hicho 2008

Mlinzi huyu wa kimataifa wa Austria ameitumikia Bayern Munich kwa miaka 13, na amekuwa akinukuliwa kuwa anandoto ya kuichezea Real Madrid na amekataa ofa 3 za The Bavarians za kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho, lakini pia alizikataa ofa za vilabu vya Liverpool na PSG ambavyo vyote vimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Kwa mujibu wa taarifa tayari Alaba na Real Madrid wameshafikia makubaliano ya awali na atasaini mkataba wa makubaliano ya awali na mabingwa hao wa kihistoria wa ulaya pindi atakapo fuzu vipimo vya afya.

Licha ya usajili wa Alaba kutajwa lakini bado haijawekwa wazi kama nahodha wa kikosi hicho Sergio Ramos ambae ndio kiongozi wa safu ya ulinzi iwapo ataondoka au atasalia klabu hapo.

David Alaba mwenye umri wa miaka 28, ameshinda jumla ya mataji 23 na kikosi cha the Bavarians ukiwemo ubingwa wa ligi kuu Ujerumani Bundesliga mara 9, ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara 2, tangu alipojiunga na mabingwa hao wa ulaya mwaka 2008.