
Trent Alexander Anorld mlinzi bora wa liverpool amekosekana katika uteuzi wa timu ya Taifa
Southgate amemuacha beki wa kulia anayeaminika kuwa bora kwa sasa miongoni mwa Waingereza wanaocheza soka katika nafasi ya ulinzi kulia,akiwa ndani ya timu ya liverpool Trent Alexander Arnold, kukosekana kwake kumezua mjadala mkubwa sana miongoni mwa wadau wa mchezo huo
Kocha huyo ametaja walinzi watatu katika nafasi hiyo, akiwemo Reece James toka Chelsea Kieran Trippier toka Atletico Madrid na Kyle Walker toka Manchester City ambaye anaamini ni bora kuliko Alexander Arnold kwa hivi sasa
Pamoja na kuachwa kwa Alexander Arnold wadau wanahoji pia kukosekana kwa Jadon Sancho wa klabu ya Borussia Dotmund ya Ujerumani aliyopo kwenye kiwango bora sana kwa sasa katika ligi ya nchi hiyo pamoja na ligi ya mabingwa Ulaya.
Katika uteuzi huwa mshtuko mkubwa kwa mashabiki umekuja baada ya kuona jina la Jesse Lingard anayeng'ara kwa sasa na klabu ya Westham akitokea Manchester United akionekana kuporomoka kabisa kiwango na tuhuma za kutokufunga goli kwa muda mrefu, lakini akiwa 'Hammers' amecheza mechi 6 na kufunga magoli 4
Timu ya taifa ya Uingereza ipo kundi I ikiwa na Hungary,San Marino,Andora Albania na Poland,wanatazamiwa kucheza michezo miwili mwishoni mwa mwezi huu 28/03/ 2021Albania na 31/03/2021 dhidi ya Poland