Jumatatu , 10th Aug , 2020

Muda mchache baada ya aliyekua Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kutangaza kujiuzulu nafasi yake na kisha kuonekana kama akiwa na viongozi wa Yanga,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo Mohamed Dewji amewataka Wanachama na Mashabiki wa Timu hiyo kuwa watulivu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba.

Mo Aliandika ''Tumetoka mbali na bado safari inaendelea; tumepita mengi Wanasimba wenzangu. Nawaomba Wanasimba wote mtulie. ''

''SIMBA SC ni kubwa kuliko mtu moja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali SIMBA. Kazi inaendelea, tuko IMARA!''