Jumapili , 9th Dec , 2018

Mchezaji wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Alikiba amepangwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha Coastal Union kinachocheza hii leo dhidi ya Mbeya City.

Alikiba akiwa na kikosi cha Coastal Union

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara TPL utakaopigwa katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, utakuwa ni wa kwanza kwa Alikiba tangu aliposajiliwa na klabu hiyo msimu huu.

Coastal Union ni timu pekee kati ya zilizopanda ligi kuu msimu huu ambayo inafanya vizuri mpaka sasa katika ligi, ambapo inakamata nafasi ya 6, ikiwa na alama 22 baada ya kushuka dimbani michezo 14.

Endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City, Coastal Union itakwea hadi nafasi ya tano au nne ikiipiku Mbeya City yenye alama 22 katika michezo 15 iliyocheza pamoja na Mtibwa Sugar yenye alama 23.

Kikosi cha kwanza cha Coastal Union dhidi ya Mbeya City ni: 1. Hussein Shariff, 2. Mbwana Hamis, 3. Abdalah Wazir, 4. Bakari Mwamnyeto, 5. Ibrahim Mohamed, 6. Athuman Chuji, 7. Issa Abushehe, 8. Mtenje Albino, 9. Andrew Simchimba , 10. Ali Kiba, 11. Ayoub Lyanga.