Ijumaa , 13th Mei , 2022

Bingwa wa zamani wa dunia kwenye masumbwi, Amir Khan ametangaza kustaafu baada ya kuutumikia mchezo huo kwa takribani miaka 27.

Amir Khan katika moja ya mapigano yake

Akiwa na umri wa miaka 35, Khan amestaafu akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 40 akishinda 34 na vipigo mara 6. Mkali huyo wa ndondi ameandika kwenye Twitter: "Ni wakati wa kutundika glavu zangu. Najihisi kubarikiwa kuwa na kazi nzuri kama hii ambayo imechukua zaidi ya miaka 27. Ninataka kusema shukrani za dhati na kwa timu nilizofanya nazo kazi,familia, marafiki na mashabiki kwa upendo na sapoti waliyonionyesha."

Khan alitwaa mataji ya dunia katika uzani wa super-lightweight na alikabiliana na nyota kama Saul 'Canelo' Alvarez na Terence Crawford katika maisha yake ya mchezo huo.

Mpiganaji huyo wa Bolton alianza safari yake ya mchezo wa masumbwi mwaka 2005 baada ya kushinda medali ya fedha ya Olimpiki katika michuano ya Athens ya 2004.

Alikua bingwa wa dunia mnamo Julai 2009, akimshinda Andriy Kotelnik kwa pointi na kupata taji la uzani wa juu wa WBA, na kisha akamsimamisha Zab Judah na kujiongezea mkanda wa IBF miaka miwili baadaye.

Kupoteza pointi zenye utata kwa Lamont Peterson kulihitimisha utawala wa Khan wa taji la dunia, na alisimamishwa na Danny Garcia alipokuwa akijaribu kushinda mikanda ya WBC na WBA katika pambano lake lililofuata. Mara ya mwisho kupanda ulingoni ilikuwa february na akapoteza dhidi ya Kell Brooky .