Ijumaa , 1st Oct , 2021

Mshindi mara tatu wa Tennisi Grandslam, Andy Murray ametolewa kwenye hatua ya 16 bora ya mashindano ya San Diego Open inayoendelea nchini Marekani baada ya kufungwa 7-5, 6-4 na Casper Ruud wa Norway.

Andy Murray akiwa uwanjani.

Murray licha ya kuanza kushinda mzunguko wa kwanza lakini alikutana na upinzani mkali uliomfanya atolewe na kuwa na kuondoka kichwa chini wakati anahaha kutafuta fomu yake ya ubora baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine, Muingereza Cameroon Norrie amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo baada ya kumfunga Muingereza mwenzake, Dan Evans7-6 (7-3) na 6-3.

Baada ya matokeo hayo, Norrie Cameroon atacheza na Denis Shapolov  usiku saa 3:45 usiku wa leo Oktoba 1, Andrey Rublev kukipiga na Shwartzman saa 5:00 usiku wa leo, Aslan Karatsev na Dimititrov Grigor watcheza saa 11:00 Alfajiri wakati Lorenzo Sonego atacheza na Casper Ruud saa 9:30 usiku wa kuamkia kesho.