Jumatatu , 29th Nov , 2021

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Afrika kwa mchezo wa Mpira wa Miguu kwa wenye Ulemavu CANAF 2021 timu ya Angola jana, Novemba 28, 2021 waliichapa Zanzibar 12-0 kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

(Timu ya Angola ya watu wanaishi na Ulemavu iliyoifunga Zanzibar 12-0)

Katika kipindi chote Angola waliutawala mchezo huo kutokana na uzoefu mkubwa wa wachezaji wao wanaocheza katika mashindano ya kimataifa.

Kipindi cha kwanza tayari Angola ilikuwa inaongoza kwa magoli sita kwa nunge na katika kipindi cha pili wakaongeza magoli mengine sita na kufanikiwa kupata ushindi wa dazani moja kwa sifuri dhidi ya timu ya Zanzibar.

Magoli ya Angola yamefungwa na Kufula Hilario, Aharo Francisco, Joachim Sabino, Chiarere Jord na Pacincia Fblio.

Wakati huo huo katika mchezo mwingine, Timu ya Siera Leone imeibamiza mabao 3- 0 ambapo bao la kwanza limefungwa katika dakika ya 15 na mshambuliaji Kuroma Ctbassy na goli la pili limefungwa dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na goli la tatu dakika ya 43 kipindi cha pili na Lumeh Foday.

Mchezo huo ulitawaliwa na mvua kubwa hali iliyosababisha kushindwa kuendelea na kwa muda baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo kumalizika kutokana na maji kujaa katika uwanja.

Mashindano haya yamezinduliwa rasmi siku ya Novemba 27 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na yatakamilika Disemba 4, 2021.