Jumatano , 16th Jan , 2019

Leo inaweza ikawa ni kumbukumbu nzuri lakini isiyokuwa na masihara ndani yake, pale ambapo watoto wa profesa wa soka aliyetamba katika klabu ya Arsenal kwa miaka 22, Arsene Wenger watakapokutana katika Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Thiery Henry na Patrick Vieira

Kwa mashabiki wa Arsenal wanakumbuka vizuri ule wakati mzuri ambao Arsenal ilifaidi matunda ya nchi kwa kushinda ubingwa wa EPL pasipo kupoteza mchezo wowote, rekodi ambayo imeshindwa kufikiwa mpaka hivi sasa licha ya kuwepo kwa vikosi bora kama Man City na Liverpool.

'Yes' ni Patrick Vieira na Thiery Henry ambao wana historia kubwa ya Arsenal na Ufaransa mgongoni mwao usiku wa leo.

Henry ni kocha wa Monaco ambayo imeporomoka sana msimu huu kiasi cha kumfukuza kocha wake, Leonardo Jadim ambaye aliwapa ubingwa timu hiyo misimu miwili iliyopita. Ina alama 14 pekee katika mechi 19 ilizocheza mpaka sasa.

Anapambana na Vieira anayekiongoza kikosi cha Nice kilicho na mtukutu kama Mario Balotelli, Nice iko katika nafasi ya 8 ya msimamo ikiwa na alama 29 katika mechi 19 ilizocheza.

Monaco ya Henry ina hali mbaya zaidi kuliko Nice ya Patrick Vieira, hali ambayo inaufanya mchezo huo kuwa ni vita kali uwanjani. Watafurahi muda mfupi wakishaingia uwanjani, saa 3 usiku wa leo lakini kitakachoendelea baada ya hapo si cha urafiki, kwani kila mmoja anahitaji alama tatu za kuokoa kibarua chake.

Bonyeza hapa chini kutazama tazidi.