Jumatano , 17th Dec , 2025

Klabu ya Arsenal imefikisha idadi ya majeruhi 100 tofautitouti na kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kwenye ligi kuu ya England kuwa na idadi kubwa ya majeruhi huku majeraha ya goti yakishika namba moja kati ya majeraha yanayowaweka nje wachezaji kwa muda mrefu .

Ben White

Vinara hao wa EPL  wamefikisha idadi hiyo Disemba 13 katika mchezo walioshinda 2-1 dhidi ya Wolves kwa Ben White kulazimika kwenda nje dakika ya 31 ya mchezo huo uliopigwa katika dimba la Emirates.

Rekodi hiyo imewekwa  kwa kipindi cha misimu miwili kuanzia  msimu 20024-2025, msimu ulioanza rasmi Agosti 16 2024, nafasi ya pili ikishikiliwa na Brighton wenye majeruhi 97 huku wapinzani wao London kaskazini Tottenham Hotspur wakishika nafasi ya tatu wakiwana majeruhi 90