Aslay alilia tuzo ya heshima

Jumanne , 13th Mar , 2018

Msanii wa Bongo fleva  Aslay amesema hajaridhika na mafanikio ambayo ameyapata kupitia mziki wake anaoufanya mpaka atakapo pata tuzo ya heshima  hapa Bongo.

Akiongea kupitia eNEWZ Aslay amesema kwamba pamoja na kufanya nyimbo nyingi hali inayopelekea wasanii wengine pamoja na mashabiki kuhisi kwamba amepata mafanikio makubwa, lakini yeye ataridhika pale atakapopata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya heshima.

Hata hivyo Aslay amesema ataendelea na staili yake ya kutoa nyimbo mfululizo huku akieleza jinsi ambavyo anajisikia furaha baada ya kuona wasanii wengine wa Bongo wanaiga staili yake hiyo.

Aidha Aslay ameweka wazi kuwa hapendi kuweka wazi mambo familia yake ndio sababu kubwa inayomfanya 'asimpost' mtoto wake wa pili na sio kwamba anazuiliwa kufanya hivyo na mpenzi wake wa sasa (Tessychocolate) kama inavyoelezwa mitandaoni.

Kwa undani zaidi usikose kutazama ENEWZ kupitia East Africa Television saa 12:00 Jioni.