
(Wachezaji wa timu ya taifa ya Australia wakishangilia kufuzu kombe la Dunia)
Australia ilitimiza ndoto yao ya kuendelea kushiriki kombe la dunia mtawalia baada ya kuilaza Peru kwa mikwaju ya penalti 5 kwa 4 katika mchezo wa mtoano kwa ngazi ya mabara.
Mlinda mlango wa Australia Andrew Redmayne, ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Mat Ryan aliyefanyiwa mabadiliko kabla ya hatua ya mikwaju ya penati, na ndiye alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa mkwaju wa mwisho wa Alex Valera.
Hii inakua ni mara ya tano mfululizo kwa Australia kushiriki michuano ya Kombe la Duniabaada ya kufuzu tangu walipofuzu mwaka 2006.Sasa Australia watakuwa Kundi D, wakipangwa pamoja na mabingwa watetezi Ufaransa, Denmark na Tunisia.
Timu ya mwisho itakayo hitimisha orodha ya idadi kamili timu zitakazo shiriki fainali za Kombe la Dunia itafahamika usiku wa leo Jumanne june 14, wakati Costa Rica itakapo minyana na New Zealand katika uwanja wa Ahmad bin Ali majira ya saa 4 kasoro usiku kwa saa za Africa Mashariki.