Mchezo huo ni sehemu ya kuwaweka wachezaji kwenye hali ya ushindani kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara (VPL) kupisha mechi za Kimataifa za kirafiki zilizo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Kwa upande mwingine Azam FC itautumia mchezo huo kama sehemu ya kujiweka vyema kuelekea mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika uwanjani hapo Machi 31 mwaka huu saa 1.00 usiku.
Mchezo huo kati ya Azam FC na Friends Rangers utapigwa majira ya saa 1:00 jioni na tayari Azam FC inaendelea na maandalizi ya mchezo huo kwa programu mbalimbali za mazoezi kwenye uwanja wake.






