
Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube
Dube ataondoka mjini Cape Town, saa 8:20 mchana, kwa ndege ya shirika la Kenya Airways, itayowasili Dar Es Salaam saa 5:45 usiku.
Aliondoka nchini Novemba 29 kwenda mjini Cape Town, Afrika Kusini, kufanyiwa upasuaji wa mkono wake wa kushoto alioumia na kuvunjika Novemba 25 kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC uliomalizika kwa Yanga kushinda 1-0.
Dube alivunjika mfupa wa Ulna, unaoanzia kwenye kiwiko hadi kidole cha mwisho cha mkono.
Alhamisi ya Disemba 3, alifanyiwa upasuaji uliofanikiwa, na anatarajia kujiuguza kwa majuma manne, kabla ya kurudi uwanjani.