Alhamisi , 9th Dec , 2021

Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta amekuwa mkali kwa wachezaji wenzake haswa wanaounda safu ya ulinzi ndani ya klabu hiyo na kuwataka kujitathmini upya kutokana na mwenendo wa kuruhusu magoli mengi katika michezo ya hivi karibuni.

 Azpilicueta 32, ametoa kauli hiyo baada ya sare ya magoli    3-3 ugenini dhidi ya Zenit St Petersburg ya Urusi huku kwenye michezo miwili mpaka sasa wakiruhusu magoli sita kwenye lango lao.

"tumekuwa imara siku zote, ndio maana haturuhusu nafasi au magoli mengi kwa wapinzani lakini kwenye michezo miwili iliyopita tumeruhusu magoli sita na kwetu sio jambo jema ,tunapaswa kulitatua jambo hili” Azpilicueta amesema 

Chelsea imemaliza nafasi ya pili nyuma ya Juventus kwenye kundi H ilhali  ni ya tatu kwenye msimamo wa Epl huku Jumamosi watakuwa Stamford Bridge wakiwakaribisha Leeds United ya mwalimu Marcelo Bielsa.