Jumatatu , 15th Jul , 2019

Mama mzazi wa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Samson Siasia, ametekwa na watu wenye bunduki leo asubuhi kwenye mji wa Odoni Bayelsa, mkoa wa  Niger Delta.

Kocha wa zamani wa Nigeria Samson Siasia

Kocha huyo amethibitisha kutekwa kwa mama yake mzazi alfajiri ya leo Julai 15, 2019, na watu wenye silaha za moto.

Siasia amesema kuwa hii sio mara ya kwanza kutekwa kwa mama yake bali iliwahi kutokea tena mwaka 2015.

Tukio hilo limetokea masaa machache tangu timu hiyo kutolewa kwenye michuano ya AFCON 2019 nchini Misri na Algeria kwenye hatua ya nusu fainali usiku wa kuamkia Jumatatu.