Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Kama ilivyokuwa kwenye tuzo za mchezaji bora wa Ulaya kwa upande wa wanaume, nyota watatu Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Virgil van Dijk, wameingia kwenye tatu bora ya tuzo za FIFA 'THE BEST'.

Tuzo ya 'THE BEST'

Shirikisho la soka duniani (FIFA), limetangaza orodha ya majina matatu ya mwisho kwa wachezaji na makocha wanaowania tuzo ya 'THE BEST' 2019.

Katika orodha hiyo FIFA imewakutanisha nguli wa soka na wapinzani wa muda mrefu Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo, ambao wiki moja iliyopita walikuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa kiume Ulaya.

Katika tuzo za UEFA wiki iliyopita Ronaldo alisema anajivunia kuwa bora kwa takribani miaka 15, akishindana na Messi huku akiweka wazi kuwa mahusiano yao ni mazuri japo anatamani siku moja wakutane kwaajili ya chakula cha usiku.

Virgil van Dijk ndio aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kiume barani Ulaya kwa mwaka 2019. Kinachosubiriwa ni kuona kama atawasimamisha tena nguli hao kwenye 'THE BEST'.

Orodha kamili ya wanaowania tuzo katika vipengele mbalimbali.

MCHEZAJI BORA WA KIUME
 

KOCHA BORA WA KIUME

 

MCHEZAJI BORA WA KIKE

KIPA BORA WA KIKE

KIPA BORA WA KIUME

TUZO YA GOLI BORA PUSKAS