Jumanne , 22nd Sep , 2020

Mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool na timu ya Uingereza Jamie Carragher anaamini kwa sasa duniani mchezaji bora ukiwaondoa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ni Kelvin de Bruyne kutokana na kiwango alichokionyesha.

Nyota wa zamani wa Liverpool, Jammie Carragher enzi za uchezaji wake.

De Bruyne alifunga bao moja na kutoa pasi ya bao la tatu katika mechi ya Manchester City dhidi ya Wolves ambapo City ilishinda kwa goli 3-1.

Alipoulizwa swali akiwa anafanya uchambuzi wa mechi hiyo juu ya nani mchezaji bora kwa sasa nyuma ya nyota hao wa Barcelona na Juventus, Jamie alisema haya.

Jammie Callagher”Kama ukiniuliza, nani nitamchagua kwenye timu yangu mchezaji bora ,jina la kwanza litakua la De Bryne.Namba anazotengeneza katika pasi zinazozaa goli na goli anazofunga ni ndoto ya mwalimu yeyote Duniani kufanya nae kazi.

Nyota huyo mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa nchini Uingereza kwa msimu uliopita, ameanzia pale alipoishia msimu uliopita.

Katika mchezo wa jana nyota huyo wa Ubeligiji alikuwa nyota wa mchezo huo kutokana kuomyesha kiwango bora sana.

TAKWIMU YA KEVIN DE BRUYNE DHIDI YA WOLVES
1 -Goli moja
4- Idadi ya mashuti yaliyolenga goli
1- Pasi iliyozaa goli
6- Nafasi alizotengeneza
6- Krosi alizopiga
5 -Kupora mpira

SAFARI YAKE YA MAFANIKIO .

Nyota huyo aliwahi kupita katika timu kadhaa ikiwemo Chelsea ambayo ilimsajili kutoka timu ya KRC Genk ya Ubeligiji, hakucheza mechi nyingi katika timu ya The Blues iliyokua ikinolewa na Jose Mourinho.

Aliuzwa katika klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani sehemu ambayo alipata nafasi ya kucheza na kuonyesha uwezo wake kama ni mmoja ya wachezaji bora wa nafasi ya kiungo duniani.

TAKWIMU ZAKE MSIMU ULIOPITA.

34- Kevin De Bryne, ndiye mchezaji aliyehusika na goli nyingi tangu mwanzoni mwa msimu uliopita alifunga goli 14 na alihusika kwenye kutengeneza goli nyingine 20 katika ligi kuu nchini Uingreza.

Kwa namba anazotengeza kila msimu na kutokuonyesha dalili za kushuka kiwango, ndicho kitu kinachomfanya Jamie Carragher aamini kwamba De Bruyne ndiye mchezaji bora duniani nyuma ya Messi na Ronaldo ambao kwa pamoja wametawala tuzo za mchezaji bora duniani kwa miaka 11.