Alhamisi , 28th Dec , 2017

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola baada ya kuipiku rekodi yake mwenyewe ya kushinda mechi 16 mfululizo akiwa na Barcelona sasa ameipiku rekodi ya Inter Milan ya kushinda mechi 17.

Guardiola na vijana wake wa Man City usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya Newcastle United na kufikisha idadi ya mechi 18 wakishinda mfulilizo.

Kwa rekodi hiyo sasa Guardiola anakuwa kocha wa kwanza kushinda mechi nyinngi katika ligi tatu kubwa barani Ulaya. Msimu wa 2010/11 alishinda mechi 16 mfululizo za La Liga akiwa na Barcelona.

Msimu wa 2013/14 alishinda mechi 19 mfululizo ndani ya Bundesliga akiwa na Bayern Munich. Na sasa ameshinda mechi 18 mfululizo ndani ya EPL akiwa na Man City.

Man City sasa inaongoza ligi kwa alama 58 ikiwa ni tofauti ya alama 15 na Man United iliyoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 43.