Jumanne , 8th Mar , 2022

Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya itaendelea usiku wa leo kwa michezo miwili ya mkondo wa pili ya mtoano hatua ya 16 bora, ambapo kalabu ya Bayern Munchen itacheza na RB Salzburg baada ya sare ya 1-1 wakati Liverpool itacheza na Inter Milan ikiwa na faida ya Ushindi wa 2-0 ugenini.

(wachezaji Robert Lwendowski na Thomas Mullar wa Bayern Munchen wakipongezana)

Kuelekea kwenye michezo hiyo, Bayern Munchen huenda ikacheza bila ya nyota wake watatu, Leon Goretzka na Corentin Tolisso wenye majeraha wakati Alphonso Davies anasumbuliwa na tatizo la moyo.

Kwa upande wa Liverpool pia wanatazamiwa kuwakosa nyota wake watatu, Robert Firmino, Joel Matip na Thiago Alcantara wenye majeraha ambayo pia yalipelekea watatu hao kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya England kwa wikiendi iliopita dhidi ya Westham United.

 (Mlinzi wa kati wa PSG Sergio Ramos)

Nayo klabu ya psg imethibitisha itamkosa tena mlinzi wake wa kati Sergio Ramos katika mchezo wao wa kesho wa ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid kutokan ana majeraha, huku Kylian Mbappe naye pia akiwa na uwezekano wa kukosekana kwenye mchezo huo baada ya jana asubuh kuumia akiwa mazoezini. Mchezo wa mkondo wa kwanza uliowakutanisha miamba hawa PSG waliibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri wakiwa nyumbani.