Jumamosi , 16th Jun , 2018

Michuano ya kumsaka bingwa wa mpira wa Kikapu yanayoratibiwa na East Africa Television LTD, kwa kushirikiana na Kinywaji baridi cha Sprite usaili umeanza leo asubuhi katika viwanja vya Mlimani City Mall ambapo utafanyika kwa siku ya leo pekee.

Afisa Masoko wa East Africa Television LTD. Basilisa Biseko amesema kuwa mechi za hatua ya mtoano kutafuta timu 16 bora utafanyika katika viwanja vya Gymkhana Posta siku ya tarehe 23 mwezi huu. 

"Usaili unaendelea hapa katika viwanja vya Mlimani City Mall ndio kwanza tumeanza timu zijitokeze kwa wingi hata kama zikifika zaidi ya Mia moja sisi tutafuta timu 16 bora ", amesema Basilisa.

Miongoni mwa wachezaji wakijisajili mapema leo

Nao baadhi ya washiriki waliokwisha jitokeza kusajili timu zao hadi sasa wameonekana wenye kujiamini kila mmoja akiahidi kufika hatua ya timu 16 bora. 

Sprite BBall Kings Inafanyikia kwa mara ya pili mara baada ya kufanya vizuri Mwaka Jana ambapo timu bingwa iliondoka na kitita cha Shilingi millioni kumi pamoja na Kombe la Sprite BBall Kings.