Jumapili , 23rd Nov , 2014

Vilabu shiriki Ligi ya Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam vimetakiwa kutokufanya usajili mpaka muda wa kufanya hivyo utakapofika.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, Richard Julles amesema hivi sasa vilabu vyote vipo mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi hiyo ambapo vilabu vitakavyoruhusiwa kufanya usajili ni vile ambavyo vitashika nafasi za sita za juu na usajili huo utafanyika ili kuongezea nguvu.

Julles amesema usajili huo utafanyika mapaka pale itakapotangazwa kuhusu usajili ikiwa ni sehemu ya kumalizia Ligi hiyo.