Jumatatu , 1st Nov , 2021

Kocha msaidizi wa Azam Fc, Vivier Bahati amesema kuwa hata kama wangekuwepo wachezaji Aggrey Morris, Salum Aboubakar na Mudathir Yahaya ambao wamesimamishwa kwa masuala ya utovu wa nidhamu lakini kipigo dhidi ya Yanga kingekuwa palepale.

Vivier Bahati-Kocha msaidizi wa Azam

Kauli ya Koch huyo raia wa Burundi inakuja kufuatia baadhi ya wakosoaji kudai kuwa kukosekana kwa nyota hao waandamizi kumechangia kwa asimilia kubwa Azam kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga ambao wana lambalamba walinyukwa bao 2-0 siku ya Jumamosi.

Akizungumzia hilo, Bahati amesema''Hata wangekuwepo wachezaji hao kipigo tusingekikwepa, bahati mbaya wachezaji wetu hawakuwa katika hali ya nzuri, na Yanga walikuwa bora zaidi yetu''. Vivier Bahati.

Ikumbukwe Azam Fc ipo katika nafasi ya 11 katika msimamo wakiwa na alama 4 katika mechi 4 waliyocheza na hawajawa na matokeo mazuri msimu huu licha ya kufanya usajili mkubwa wa wachezaji.

Ikumbukwe Morris, Mudathir na Morris walisimamishwa kutokana na masuala bila kikomo kufuatia masuala ya utovu wa nidhamu.