Jumamosi , 26th Apr , 2014

Shirikisho la Masumbwi Tanzania, BFT limesema limeshapeleka majina ya mabondia watakaoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola katika Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)

Mabondia wa Ngumi za Ridhaa katika moja ya michuano nchini Tanzania

Shirikisho la Masumbwi Tanzania, BFT limesema limeshapeleka majina ya mabondia watakaoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola katika Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC ili kuhakikiwa tayari kuelekea nchini Scotland katika michuano hiyo inayotimua vumbi Mwezi July, mwaka huu.

Katibu wa BFT, Makore Mashaga amesema Mabondia wanaendelea kujiandaa kwa mwezi wa tatu sasa wakisubiri TOC kutangaza tarehe ya kuanza safari kuelekea katika michuano.

Mashaga amesema bado kunachangamoto kubwa ya udhamini kutokana na uhaba na ukosefu wa vifaa mabondia wanashindwa kujiandaa vilivyo ikiwa ni pamoja na kupata chakula .