Jumatano , 27th Mei , 2020

Katika taarifa iliyotolewa kupitia kwa Katibu Mkuu, Neema Yotham imesema kuwa BMT imetoa taarifa kwa michezo mingine kuwasilisha taarifa kuhusu programu zao za kurejea zikieleza watazifanya lini na kwa utaratibu gani.

BMT

"Programu zao zinapaswa pia zionesha ni mkakati gani watauchukua katika kudhibiti maambukizi kwa sababu Mhe. Rais amesema tuendelee na taratibu zetu lakini tuchukue tahadhari", amesema Neema.

"Baada ya kuwasilisha tutakaa BMT kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa ajili ya kutengeneza mwongozo wa namna gani tutazitekeleza hizo program za michezo mingine", ameongeza.

Mtazame hapa akizungumza zaidi.