
Bondia Marvin Hagler 'Marvelous'
Katika wakati huo Hagler alipigana mapambano 67, akishinda 62 huku 52 ikiwa ni kwa KO. Sare mara 2 na kupigwa mara 3.
"Leo, kwa bahati mbaya mume wangu mpendwa Marvelous Marvin amefariki bila kutarajia nyumbani kwake hapa New Hampshire," amethibitisha mkewe Kay Hagler.
Ikumbukwe mnamo Septemba 1980, Hagler alipambana na Alan Minter wa Uingereza kwenye Uwanja wa Wembley kupambania mataji yake ya kwanza ya Ulimwengu na akashinda mikanda ya WBA na WBC.