Jumamosi , 10th Jan , 2026

Nyota wa timu ya taifa ya Morocco, Brahim Diaz, ameendelea kung’ara katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kuandika rekodi mpya barani Afrika baada ya kufunga bao katika mechi tano mfululizo.

Brahim Diaz

Kwa rekodi hiyo, Brahim Diaz amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi 5 mfululizo za AFCON tangu mwaka 1968, jambo linalomuweka kwenye orodha ya wachezaji wachache waliowahi kufanya makubwa katika historia ya mashindano hayo.

Diaz ameonyesha kiwango cha juu katika kila mchezo aliocheza, akionesha uwezo mkubwa, kasi na umakini mbele ya lango. Mabao yake yamekuwa na mchango mkubwa katika safari ya Morocco kwenye michuano hiyo, huku mashabiki na wachambuzi wakimtaja kama mmoja wa wachezaji bora wa AFCON 2025.

Rekodi hii inabaki kuwa ya kipekee, kwani katika historia ya michuano hiyo hakuna mchezaji aliyewahi kufunga bao katika mechi tano mfululizo.

Katika historia ya mashindano ya AFCON, Laurent Pokou wa Ivory Coast aliwahi kufunga mabao 6 mwaka 1968, lakini hakufunga mfululizo kama Brahim Diaz.

Gwiji huyo anabaki kwenye rekodi ya mashindano haya makubwa barani Afrika kwani ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi kabla ya kustaafu.