Jumamosi , 4th Jun , 2022

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United, Manchester City, West Ham United, Juventus na Timu ya taifa ya Argentina Carlos Tevez amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 38.

Tevez ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu England EPL mara 3

Tevez amesema kufariki kwa baba yeke mzazi ni sababu iliyomfanya astaafu kucheza soka, ingawa amekuwa akipokea ofa za timu nyingi kutaka kumsajili.

"Niliacha kucheza kwa sababu nilipoteza shabiki wangu namba moja (baba yeke). Nimestaafu, imethibitishwa, nimepata offa nyingi ikiwemo kutoka Marekani. Kucheza mwaka jana ilikuwa ngumu sana.”Amesema Tevez

Baba mzazi wa Tevez Segundo Tevez alifariki Februari 2021 akiwa na umri wa miaka 58. Tevezi hajaonekana uwanjani akicheza tangu mwezi Juni mwaka jana 2021. Katika kipindi cha takribani miaka 20 Tevez amevichezea vilabu takribani 7 tofauti na ameshinda makombe 25 ngazi ya klabu ikiwemo ubingwa wa Ligi kuu England EPL, Italia Seria A, na amecheza jumla ya michezo 746 na amefunga mabao 308.