
Wapinzani wa Yanga katika kombe la klabu bingwa Barani Afrika,Cercle De Joachim kutoka Mauritius wanatarajiwa kuwasili nchini kuanzia jumatano au Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kombe la klabu bingwa Barani Afrika jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya Yanga Jerry Murro amesema tayari Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limeshatuma majina ya waamuzi watakao chezesha mchezo huo,ambao Yanga inahitaji matokeo yoyote ya sare baada ya kushinda mechi ya raundi ya kwanza huko Mauritius wiki mbili zilizopita.
Katika kujiandaa na mechi hiyo,Murro amesema tayari kikosi chao kimeshaanza kambi kwenye chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kesho Yanga inaingia uwanjani kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la TFF dhidi ya KJT Mlale,mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,kisha itaendelea na kambi hiyo hadi jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Cercle De Joachim.
Mchezo huo wa marudiano,Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele,kufuatia kushinda bao 1-0 kwenye mchezo uliopita wiki mbili nyuma huko Mauritius.