
Matabibu wa Chelsea wamethibitisha taarifa hiyo baada ya kuumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, katika mchezo dhidi ya Juventus kwenye ushindi wa 4-0.
Mabingwa hao wa ulaya wanalazimika kuingia sokoni kutafuta beki ambaye atasaidiana na Marcos Alonso, ambapo mpaka sasa Chelsea wanaisaka sahihi ya beki wa Everton, Mfaransa Lucas Digne aliyekuwa tofautiana na kocha Rafael Benitez.
Iwapo Usajili wa Digne utashindikana, Chelsea watalazimika kuwarudisha mabeki wao wa kushoto waliopo kwa mkopo, Emerson Palmiera anayetumikia Klabu ya Lyon kutoka nchini Ufaransa na kinda Ian Matseen,20, raia wa Uholanzi anayecheza ligi daraja la kwanza akiwa na Coventry City.
