Chirwa atuma ujumbe kwa Wanayanga

Jumatano , 14th Feb , 2018

Nyota wa kimataifa wa Yanga Obrey Chirwa amewaandikia ujumbe mzito mashabiki wa soka nchini hususani wale wa klabu yake ya Yanga baada ya kuonekana kumbeza anapokosa Penalti.

Chirwa ameuonesha ujumbe huo ulioandikwa kwenye fulana aliyokuwa amevaa ndani ya jezi yake kwenye mechi inayoendelea dhidi ya Majimaji baada ya kufunga bao lake la 11 msimu huu dakika ya 30.

Ujumbe huo unasomeka ''Never Give Up'' ambao kwa tafasri sahihi ya kiswahili ni ''Usikate tamaa''. Hii inakuja ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu akose Penalti kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis jumamosi iliyopita.

Chirwa kwasasa ndiye anaongoza kwa mabao ndani ya Yanga akiwa amefikisha mabao 11 akiwa nyuma ya okwi mwenye mabao 13 huku akimzidi John Bocco mwenye mabao 10.

Mechi ya Yanga SC dhidi ya Majimaji FC inaendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo ni dakika ya 60, Ynaga inaongoza 3-1.