
Lukaku kulia akiwa na kocha Antonio Conte
Lukaku mwenye umri wa miaka 27, raia wa Ubeligiji ameshaifungia Inter Milan mabao 25 msimu huu kwenye michuano yote bao 19 kati ya hayo amefunga kwenye ligi kuu Serie A’ na ametoa pasi za usaidizi wa mabao 7. Kutokana na kiwango bora alichonacho sasa vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya vimeonyesha nia yakuhitaji huduma yake, timu zinazotajwa ni Real Madrid, FC Barcelona, Manchester City na timu yake ya zamani Chelsea.
Maelewano mazuri kati yake na kocha wake Antonio Conte ndio sababu inayotajwa kuwa itamfanya mshambuliaji huyo kusalia katika klabu hiyo ya Jijini Milan nchini Italia na inaripotiwa kuwa endepo kama Kocha Conte ataondoka basi Lukaku nae atajitathimi juu ya hatima yake juu ya wapi aelekee.
Mkataba wake na Nerazzurri unamalizika mwaka 2024, na kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia ni kwamba Inter wamejipanga kumpa mkataba mpya ambao utakuwa na ongezeko la mshahara.
Inter ndio vinara wa ligi kuu nchini Italia Serie A’ msimu huu wakiwa na alama 65 tofauti ya alama 6 namajirani zao AC Milan walio nafasi ya pili wakiwa na alama 59. Mara ya mwisho kikosi hicho kutwaa ubingwa wa ligi kuu ilikuwa msimu wa 2009-10.