Rais wa CAF, Ahmad Ahmad akihutubia moja ya mkutano wao
''Asubuhi ya leo nimethibitika kuwa na maambukizo ya Corona, sina dalili yoyote inayoonekana lakini vipimo vimeonesha hivyo''
Aliongeza kuwa '' nitalazimika kujitenga kwa siku 14 kama kanuni inavyosema,ili kujipa muda wa kutosha niweze kurejea katika hali nzuri na kurudi kwenye majukumu yangu ya kila siku'' alisema Ahmad
Ahmad raia wa Madagasca mwenye umri wa miaka 60 ambaye aliingia madarakani mwaka 2017, baada ya kumuangusha Issa Hayatou anakabiliwa na changamoto kadha kwenye uongozi wake ndani ya CAF
CAF wanatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi mapema mwaka 2021 nchini Morocco, huku Ahmad Ahmad akiweka wazi dhamira yake ya kuwania tena nafasi hiyo