
Wachezaji wa timu ya taifa ya Costa Rica wakishangilia baada ya kufuzu kombe la Dunia
Ni kwa mara ya 3 mfululizo Costa Rica wanafuzu kucheza kombe la Dunia na wamekata tikeki hii jana usiku baada ya kuifunga timu ya taifa ya New zealand bao 1-0 kwenye mchezo huo wa mtoano ambao ulihusisha timu kutoka Marekani Kaskazin na bara la Ocean bao pekee la mchezo huu limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Joel Campbell.
Taifa hili la Costa Rica kutoka Marekani Kaskazini imekamilisha idadi ya timu za mataifa 32 zitakazochuana kuwania ubingwa wa Dunia katika fainali zitakazo anza kutimua vumbi Novemba 21 hadi Disemba 18, 2022 nchini Qatar. Na wamepangwa kundi E lenye timu za Japan, Hispania na Ujerumani.
Fainali za kombe la Dunia za mwaka 2014 ndio zilikuwa fainali zao bora kabisa, walifanikiwa kufika hatua ya robo fainali. Baada ya kumaliza vinara wa kundi ambalo lilikuwa na mataifa ya Engand, Italia na Uruguay wakaitoa Ugiriki hatua ya 16 bora kabla ya kutolewa na Uholanzi hatua ya robo fainali.