
(Mcheza tennis wa Argentina, Juan Martin Del Potro )
Del Potro (33), amepoteza dhidi ya Federico Delbonis kwa kufungwa 6-1 na 6-3 katika michuano ya wazi ya Argentina na baada ya kumalizika kwa mchezo huo alibubujikwa na machozi na kubembelezwa na Delbonis baada ya kichapo hicho.
"Sidhani kama tutaweza kuonana tena maana napaswa kuongea na madaktari wangu kujua hali yangu ya kiafya na napaswa kuangalia vizuri mguu wangu na tutaona kipi kitajiri lakini kama leo itakuwa siku yangu ya mwisho basi nitakuwa na furaha pia maishani mwangu" Amesema Del Potro akiwahutubia umati uliojitokeza mjini Buenos Aires.
Martin Del Potro alivunjika mguu mnamo mwaka 2019 na kufanyiwa upasuaji mara tatu wa mguu wake huku mapema mwaka huu alitangaza kama atastaafu mchezo wa tennis basi atatumia mashindano ya wazi ya Rio yatakayofanyika nchini Brazil kuwaaga mashabiki wake.