
Ousmane Dembele
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alichukua jukumu muhimu katika msimu wa kihistoria wa klabu yake, ikiwa ni pamoja na kutoa pasi mbili za mabao katika wa 5-0 dhidi ya Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Munich
"Sikutaka kulia, lakini mara tu nilipoanza kuzungumza juu ya familia yangu, juu ya watu ambao wamekuwa wakinisaidia, iliibuka na sikuweza kuizuia," Dembele aliambia Reuters baadaye.
Mchezaji huyo wa zamani wa Dortmund aliweza kuhudhuria hafla ya utoaji tuzo huko Paris ingawa PSG walikuwa wakicheza na Marseille Jumatatu usiku kwa sababu ya jeraha la misuli ya paja. Alizidiwa na hisia alipokabidhiwa kombe, na akamleta mama yake jukwaani kufurahia wakati huo pamoja.
Nyota chipukizi wa Barcelona Lamine Yamal alimaliza wa pili lakini pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa U21.